RAIS MAGUFULI AMEVUNJA KAMISHENI YA TUME YA VYUO VIKUU (TCU)

Image result for tume ya vyuo vikuu tanzania

RAIS John Magufuli amevunja Kamisheni ya Tume vya Vyuo Vikuu (TCU) na kuwasimamisha kazi watendaji wakuu wa tume hiyo baada ya kubainika kudahili wanafunzi wasio na sifa na kuwapa mikopo.

Pia serikali imetangaza kufanyika kwa udahili upya Vyuo Vikuu vyote nchi nzima ili kuwaondoa vyuoni wanafunzi wote wasio na sifa sambamba na kutangaza vita kali kwa wanafunzi hewa wanaopata mikopo ya elimu ya juu.


Hayo yamebainishwa leo na Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habali juu ya kuvunjwa kwa Kamishina ya TCU.

Amesema, kwa idhini aliyopewa na rais anawasimamisha kazi mara moja watendaji hao wa Kamisheni ya Tume ya Vyuo Vikuu.

Prof. Ndalichako amewataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Prof. Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa kushindwa kusimamia kazi za TCU akiwa kama mtendaji mkuu wa taasisi hiyo.

Pia, Dk. Savius Maronga, Mkurugenzi wa Udhibiti na Ubora kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kusimamia ubora na ithibati ya Vyuo Vikuu.

Amesema Rose Kiishweko, Mkurugenzi wa Udahili amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia udahili wa wanafunzi na kupelekea kudahiliwa wanafunzi wasio na sifa, na mwingine aliyesimamishwa ni Kimboka Istambuli ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka.

Image result for tume ya vyuo vikuu tanzania

Mbali na hilo Prof. Ndalichako amesema, ili shughuli za TCU ziendelee, Prof. Eliuter Mwageni ameteuliwa kukaimu nafasi ya katibu mtendaji na kabla ya uteuzi wa kukaimu nahfasi hiyo Prof. Mwageni alikuwa Naibu Makamu Mkuu (Utawala na Fedha) wa Chuo Kikuu cha Ardhi.

Aidha ameteuliwa Dk. Kokubelwa Mollel ambaye atakaimu nafasi ya ukurugenzi wa udahili na nyaraka na kabla ya uteuzi wa kukaimu nafasi hiyo Dk. Kokubelwa alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph wanaodahiliwa kutokuwa na sifa.

Waziri amesema, kutokana na hilo serikali imeamua kutoa tamko baada ya ukaguzi kufanyika katika chuo hicho katika kampasi za Arusha na Songea na kubaini kuwepo kwa upungufu mkubwa katika utoaji wa elimu isiyokuwa na kiwango.

banner
Previous Post
First